loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Wawili mbaroni tuhuma za ujambazi

Akitoa taarifa za kukamatwa kwa watuhumiwa hao jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita alisema Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwatia mbaroni majambazi hao Oktoba 14 mwaka huu majira ya saa nne usiku, katika daraja la Holili lililopo kata ya Holili wilayani Rombo.

Moita alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao, kumetokana na matukio mbalimbali ya ujambazi ambayo yamekuwa yakitokea, katika wilaya za Rombo na Moshi Vijijini, hali iliyolazimu jeshi la polisi kufanya msako mkali wa kuwabaini na kuwatia mbaroni.

Kamanda Moita bila kuwataja majina ya watuhumiwa hao kwa sababu za kipelelezi, alisema baada ya kuwakamata, walihojiwa ambapo wakiwa chini ya ulinzi waliwaongoza polisi hadi eneo walilokuwa wameficha silaha.

Alisema upekuzi ulifanyika na kufanikiwa kukamata silaha mbalimbali zikiwemo za moto, jadi na risasi tisa, zikiwa zimefichwa chini ya daraja la Holili, ambapo alizitaja kuwa ni shotgun yenye namba 13704 ikiwa na risasi tatu na bunduki aina ya SAR yenye namba AF.3811 ikiwa na risasi sita.

Alitaja vitu vingine vilivyokamatwa ni pamoja na mapanga mawili, sime moja, kofia tatu za kuficha sura, simu za mawasiliano 17, funguo za pikipiki 17, vocha za simu za mitandao mbalimbai pamoja na fedha ambazo hazikutajwa kiwango chake.

foto
Mwandishi: Arnold Swai, Moshi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi