Mpaka sasa jumla ya washindi 37 wameshapatikana kutoka katika mikoa mbalimbali.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari hayo, Meneja wa Airtel Kanda ya Kaskazini, Brighton Majwala alisema amefurahisha sana na kupatikana kwa washindi kutoka katika kanda hiyo.
Alisema anajivunia Airtel kwa kuwa sehemu ya kubadili maisha ya Watanzania wengi hasa walio na kipato cha chini na kuwawezesha kufikia ndoto zao huku kwa kurahisisha shughuli zao za kiuchumi na kijamii kupitia promosheni.
Kwa upande wake Mohamed Ahmad Khamis alisema amejisikia furaha kubwa kutimiza ndoto na akiwa mtumiaji mzuri wa huduma za Airtel ataendelea kuzitumia.