loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wazalishaji wa bidhaa za ndani wanastahili pongezi

Pamoja na hilo, Rais Kikwete alisema kwa ubora aliouona, ni dhahiri kuwa nchi yetu inapiga hatua kuweza kushindana katika masoko mbalimbali duniani.

Aliongeza kuwa kinachotakiwa sasa ni kuboresha zaidi ubora wa bidhaa na vifungashio, huku akisema kwa sasa nchi inaweza kujivunia bidhaa zilizopo katika soko la ushindani.

Mbali ya Rais Kikwete, viongozi mbalimbali waliotembelea maonesho ya mwaka huu, tangu yalipoanza Juni 28, walieleza kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika maandalizi yake, lakini pia katika ubora wa bidhaa za ndani zinazooneshwa katika maonesho hayo, unaotoa ushindani katika ngazi ya kimataifa.

Pongezi hizo zilizotolewa na Rais Kikwete na viongozi wengine ni salamu tosha kwa wazalishaji hao wa bidhaa za ndani, kubaini kuwa jitihada wanazozifanya katika kuboresha bidhaa zao, zimefikia katika kiwango kinachokubalika kimataifa hivi sasa.

Kilio cha bidhaa za Tanzania kwa miaka yote ya Maonesho ya Sabasaba, kilikuwa ni ubora hafifu, unaodidimizwa zaidi na vifungashio hafifu, hatua ambayo mara zote ilikuwa inazifanya bidhaa hizo kushindwa kutoa ushindani katika ngazi ya kimataifa.

Ni tumaini letu sasa wazalishaji wa ndani watatumia salamu hizi za Rais Kikwete juu ya ubora wa bidhaa zao, kama motisha chanya ya kuendelea kuboresha bidhaa hizo, zaidi ya ilivyo sasa ili kuwafanya kushika namba moja katika ushindani wa soko la kimataifa.

Tunasema hivyo kutokana na changamoto iliyopo katika masoko ya kikanda, kama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), lakini pia Umoja wa Ulaya (EU) na katika ngazi nyingine za kimataifa.

Ubora kwa bidhaa za Tanzania, itakuwa ndio njia pekee ya kuifanya Tanzania kuweza kushindana na nchi kama Kenya, yenye ukuaji wa viwanda unaofikia asilimia 80, ndani ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki, hasa kutokana na Itifaki ya Ushuru wa Forodha inayolinda bidhaa za ndani ya jumuiya kutolipiwa ushuru wowote, kama njia ya kuwainua wazalishaji na bidhaa za ndani.

Pamoja na hayo, ni matumaini yetu kuwa wazalishaji hawa wa ndani, pia watazingatia ushauri wa Rais Kikwete wa kuendelea kuboresha bidhaa zao, badala ya kubweteka, kwani ukuaji wa sayansi na teknolojia umefanya kuwepo na changamoto za kuinua ubora wa bidhaa katika kila siku iendayo kwa Mungu.

Kwa kuwa na bidhaa imara na bora zinazoendelea kuboreshwa kila siku, kutaifanya Afrika na Dunia kuitazama Tanzania kwa jicho la aina yake katika uzalishaji wa bidhaa.

Hatua hiyo inaweza kuvutia uwekezaji wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kwa kiwango kikubwa, na kuiwezesha Tanzania kutimiza ndoto ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

UCHAGUZI Mkuu wa madiwani, wabunge, wawakilishi, Rais wa Zanzibar na ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi