loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wazawa Afrika Mashariki watakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi

Aliyasema hayo jijini Mwanza wakati alipofungua maonesho ya nane ya kibiashara kwa nchi za Afrika Mashariki.

Alisema amevutiwa na maonesho hayo ambayo yanatumika pia kuwaunganisha pamoja wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kiuchumi, kifikira na mtangamano wa pamoja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wenye Viwanda, Biashara na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Mwanza, Elibariki Mmari alizitaka serikali za nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuondoa vikwazo vya kiuchumi vilivyo katika nchi hizo vinavyominya ukuaji wa uchumi katika nchi hizo.

Aliwataka wafanyabiashara wa nchi za Afrika Mashariki kushirikiana na TCCIA ili kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kwa kubadilishana taarifa mbalimbali za kibiashara kwa wafanyabiashara wa nchi hizo na nchi zingine.

Mmari alisema maonesho hayo yameendelea kupata umaarufu kutokana na idadi ya washiriki kuongezeka mwaka hadi mwaka, ambapo mwaka 2006 wakati yanaanzishwa yalikuwa jumla ya washiriki 80 na mwaka jana washiriki 320.

“Na kwa mwaka huu kuna washiriki zaidi ya 350 kutoka nchi za Kenya, Uganda, India, Korea na wenyeji Tanzania”, alisema.

Kiuchumi, alisema kwa mwaka jana maonesho hayo yaliweza kuuza biashara za papo kwa papo zenye thamani ya Sh milioni 380 na biashara za oda zilizokusanywa ziliweza kufikia thamani ya Sh milioni 250.

MCHICHA ni aina nyingine za ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi