loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Wazazi Nipendeni’ awamu ya pili yazinduliwa Dar

Kampeni hiyo safari hii inamhusisha mwaka mmoja wa kwanza wa maisha ya mtoto.

Uzinduzi huo ulifanywa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Neema Rusimayila katika viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, Dar es Salaam.

Uzinduzi huo umefanyika baada ya awamu ya kwanza kupata mafanikio makubwa.

Alisema kampeni hiyo imesaidia kupunguza vifo vya wajawazito, watoto wachanga na pia kuhakikisha watoto wanaozaliwa wana afya njema kwa kuhakikisha kina mama na wenza wao wanafuata hatua zote za afya ya uzazi.

“Hapa Tanzania, idadi ya vifo vya watoto ni 51 kwa kila 1,000 wanaozaliwa ambayo bado ni kubwa ikilinganishwa na malengo ya serikali kupunguza idadi hii hadi wanne kwa kila 1000 wanaozaliwa,” alisema.

Alisema kutokana na azma hiyo, kuna haja ya kuendelea kuweka nguvu katika kampeni hiyo na kutaka mikoa yote na halmashauri zake kuhakikisha wanaipa kampeni hiyo kipaumbele na kuitekeleza ipasavyo ili kuhamasisha kina mama na wenza wao kufuata hatua za afya ya uzazi.

“Tunaamini kuwa awamu hii ya pili itaharakisha upatikanaji wa habari kuhusu uzazi wa afya ili kupunguza vifo,“ alisema na kuongeza kuwa Chuo Kikuu cha John Hopkins pia kimeungana na Shirika la USAID na wizara pamoja na wadau wengine katika kutekeleza awamu hiyo ya pili.

Mwakilishi wa Shirika la USAID, Ana Badipo-Memba alisema wameridhika na mafanikio yaliyopatikana katika kampeni hiyo.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi