loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wazazi, vijana tumieni fursa siku ya tenisi

Tanzania, wameona waadhimishe leo ili kuipa jamii fursa ya kushiriki kikamilifu kwa maana Machi 3 ni siku ya kazi. Katika mahojiano maalumu na Kocha wa timu ya Taifa ya Tenisi, Kyango Kipingu, anasema, siku hiyo ni muhimu kwa jamii kujitokeza kwa wingi na kujifunza jinsi ambavyo mchezo huo ni muhimu katika maisha.

Anasema ni ajira kubwa kwa vijana, hivyo ni fursa ya pekee kwa Watanzania kujitokeza siku hiyo kwenye uwanja wa Gymkhana kuungana nao katika kucheza. “Ni siku muhimu kwetu kama wachezaji na viongozi wa mchezo huu kusherehekea kwa kucheza na kukaribisha wale wapya, waone tunafanya nini,” anasema.

Kyango anasema, hii ni mara ya kwanza kwao kuadhimisha siku hiyo ambapo wanahamasisha watu wapya wasioujua mchezo huo, na ambao wanatamani kujifunza kutumia nafasi hiyo ya kwenda kushuhudia. “Tunapenda kuwaalika watu wa rika zote, ni nafasi ya pekee kwao, kuja kucheza ikiwa ni sehemu ya kusherehekea, tutatumia vifaa vichache vilivyopo katika kuwafundisha wale watakaopenda,” anasema.

Anasema, kwa vile ni siku muhimu hakuna kiingilio chochote, kama ambavyo wengi wamekuwa wakifikiri. Kyango anasema, wakati yeye na wanamichezo wengine wanaadhimisha siku hiyo muhimu, anawakumbusha watu kutambua kuwa tenisi ni maisha, ajira na kuongeza kuwa siku zote atabaki katika mchezo huo kuhamasisha watoto kwenye shule na vijana kujiunga kusudi kuongeza idadi kubwa ya wachezaji wapya.

Mpango wa Chama cha Tenisi Tanzania (TTA) ni kuhakikisha kuwa inaendelea kuongeza idadi ya wachezaji wa kike na wa kiume kwani bado ni wachache. Kyango anazungumzia hilo kama changamoto katika timu ya Taifa, kutokana na idadi ya wale alionao kuwa ndogo kwenye kikosi chake. Wengi waliopo ni vijana wa kiume.

Wachezaji wengi waliopo katika kikosi chake ambao wamekuwa wakifanya vizuri hutoka Arusha pekee. Hiyo ni changamoto kubwa kwake kuangalia uwezekano wa kwenda kwenye mikoa kutafuta wengine wenye uwezo na vipaji vipya. Kuhusu mpango huo, Kyango anasema tayari ameanza mchakato wa kuzunguka kwenye shule na kufundisha walimu na wanafunzi mchezo huo.

Aidha, wakati wanafikiria kufanya hivyo wanakabiliwa na uhaba wa viwanja kwa ajili ya mchezo huo. Ndio maana katika shule nyingi za serikali wengi wamekuwa wakicheza mpira wa miguu na netiboli pekee. Kingine kinachowakabili ni fedha za kufanikisha mipango hiyo. Makamu Mwenyekiti wa TTA, Fina Mango, anasema katika kufanikisha kile wanachokusudia wataenda katika mikoa mbalimbali hasa ile yenye viwanja na kufanya kliniki ya kutafuta wachezaji.

Pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo, wanalo la kusherehekea na kubwa wanalojivunia ni kufanya vizuri kwa timu ya Taifa ya vijana kwenye mashindano mbalimbali makubwa. Hivi karibuni kulikuwa na Mashindano ya Afrika Mashariki yaliyofanyika kwenye uwanja wa Gymkhana ambapo waliwezesha Tanzania kushika nafasi ya pili.

Timu hiyo ya Taifa kwa sasa iko Nairobi, Kenya ikijifua kuchuana kwenye mashindano ya Afrika yatakayoanza hivi mwezi huu. Lakini wakati Tanzania ikisherehekea kwa kujivunia baadhi ya mafanikio hayo, kwa upande mwingine Shirikisho la Tenisi Duniani (ITF) nao pia wataungana na wachezaji maarufu kesho kutwa kwa ajili ya kusherehekea.

Kwa mujibu wa mtandao wa ITF, wachezaji maarufu duniani watakutana katika miji mitatu HongKong, London na New York. Kwa mujibu wa mtandao huo, siku hiyo imeandaliwa kwa lengo la kutangaza mchezo huo na kwamba miongoni mwa wachezaji kutoka mataifa 60 duniani wamethibitisha kushiriki katika kusherehekea.

“Wachezaji maarufu wa sasa na wale wastaafu pamoja na chipukizi na wachezaji wenye ulemavu ikiwahusisha wale wanaofahamika na ITF watashiriki kufanya kampeni za mchezo huo,” inasema taarifa ya mtandao huo.

Kutakuwa na baadhi ya wachezaji maarufu kama Tomas Berdych, Lleyton Hewitt, Li Na na Samantha Stosur ambao watacheza mashindano yanayofahamika kama BNP Paribas katika mji wa Hong Kong. Wakati huohuo, Andre Agassi, Pete Sampras, Pat Cash na Ivan Lendl watakuwepo katika mji wa London.

Wengine watakaocheza siku hiyo ni Novak Djokovic, Andy Murray, Bob Mike Bryan, John na Patrick McEnroe ambao wamepangiwa kucheza katika mji wa Newyork. ITF inahamasisha vyama vya tenisi vya duniani kutumia siku hii kuhamasisha watu kuunga mkono lakini pia kucheza kuanzia ngazi ya vijiji hadi taifa.

Wanasema hiyo ndio siku pekee ya kuutangaza mchezo huo ili kuchezwa na wengi. Kufanya hivyo ni sehemu ya kuunga mkono kampeni yao waliyozindua mwaka 2007 iliyolenga kuongeza ushiriki wa wachezaji wa mchezo huo duniani.

MKUU wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Godwin ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi