loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Waziri aahidi kuwatafutia masoko wafanyabiashara wa ng’ombe

Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Titus Kamani, aliyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa ng’ombe wilayani Kahama katika ziara yake ya siku moja wilayani hapa.

Kamani alisema Wizara yake ipo tayari katika kuwasaidia wafugaji wa ng’ombe katika kuwatafutia masoko katika nchi mbalimbali ili waweze kufanya biashara ya ushindani zaidi kuliko ilivyo kwa sasa kwani wafanyabiashara hao wamekuwa watumwa na wale wa nje.

Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Busega, aliwatahadharisha wafugaji hao kuacha kuuza ng’ombe wakiwa bado ni wazima kwani wanapoteza mali nyingi ikiwemo ngozi, Pembe pamoja na nyama hali ambayo inawanufaisha wale wafanyabiashara wa nje.

Awali katika taarifa yake, Mwenyekiti wa Chama cha Wanenepeshaji ng’ombe wilayani Kahama, John Nyenye alisema wanapata changamoto kubwa katika kufanya biashara hiyo ikiwa ni pamoja na kukosa soko la ndani la uhakika hususani katika migodi iliyopo wilayani hapa.

Nyenye alisema wao kama wafanyabiashara wa ng’ombe wanatumia muda wa siku 90 kwa kuwanenepesha ngombe hao huku wakiwanunua kwa bei ya kuanzia Sh milioni moja, katika wilaya za Geita na Ngara huku wenyewe wakiwauza kati ya Sh milioni 1.6.

Nyenye alisema kuwa changamoto nyingine ni sehemu za malisho ya ngo’mbe hao na upatikanaji wa maji kwa ajili ya mifugo kunywa, na aliongeza kuwa mpaka kufikia hivi sasa bado Halmashauri ya Mji haijawatengea maeneo ya malisho.

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imetangaza ...

foto
Mwandishi: Raymond Mihayo, Kahama

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi