loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri Chikawe ataka uharaka uwasilishaji majina ya wabunge

Chikawe aliyasema hayo jijini Dar es Salaam huku akisisitiza kuwa, muda uliobaki ni mdogo hivyo ni vyema kuwahisha ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baada ya muda wa ukomo kufika.

Kwa mujibu wa Chikawe, mwisho wa kupeleka majina Ikulu ni Januari 2, hivyo makundi yaliyosalia yautumie vizuri muda uliopo kuhakikisha yanapata wawakilishi katika Bunge hilo la Katiba linalotegemewa kuundwa baada ya Tume ya Marekebisho ya Katiba kuvunjwa hivi karibuni.

“Taarifa nilizonazo ni kwamba kuna makundi hayajapeleka mapendekezo ya majina ya wawakilishi wao Ikulu hadi sasa, wavuvi waliniambia wangepeleka jana (Jumamosi) hivyo nawakumbusha wote wanaopaswa kufanya hivyo waharakishe kwa sababu siku zilizobaki kuanzia leo (jana) ni sita tu”, Chikawe alisema.

Aliwakumbusha kuwa wanaweza kupeleka majina hayo kwa njia mbalimbali ikiwemo kuyatuma kwa Katibu Mkuu Kiongozi Bara au Zanzibar au kuyawasilisha kwa viongozi hao wao wenyewe.

“Chamsingi ninachoomba kwa makundi husika ni kuzingatia kutuma majina yenye uoanisho wa dini, jinsi, kabila ili kuondoa uwezekano wa kuwa na wawakilishi wa kabila fulani au dini fulani pekee, hivyo kutotengeneza uwakilishi wenye sifa ya utaifa. “Mpeni Rais nafasi ya kutengua mapungufu hayo kama yatajitokeza kwenye mapendekezo ya majina yenu. Fanyeni hivyo kwa kumpa majina mengi, mfano kundi linalopaswa kuwa na wawakilishi 20 litume hadi majina 80 ili kama la watu 20 wa kwanza litakuwa na Wasukuma watupu au kabila fulani pekee aweze kutengua na kubadili baadhi kutoka katika majina ya ziada yaliyopendekezwa,” alisema Chikawe.

Akizungumzia makabidhiano ya rasimu hiyo, Chikawe alisema yatafanyika mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Mohammed Shein katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.

“Pamoja na rasimu hiyo, Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Joseph Warioba atakabidhi pia taarifa ya Tume yake itakayoeleza mambo mbalimbali yaliyojitokeza katika mchakato wa marekebisho ya Katiba, changamoto walizozipitia pamoja na mapendekezo ambayo Tume inaona yanafaa kuwepo kwenye Katiba hiyo,” alisema Chikawe.

Katika majina hayo yatakayopendekezwa kutoka katika makundi ya kidini, vyama vya siasa na taasisi zisizo za Serikali (NGOs) yataunda kundi la watu 201 watakaoteuliwa na Rais kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba, wengine 357 ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati 76 wengine watatoka katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema maeneo mengi ...

foto
Mwandishi: Namsembaeli Mduma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi