loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri Mgimwa kuzindua Mwanamitindo wa Utalii

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mratibu wa shindano hilo Samuel Malugu, alisema sherehe za uzinduzi zinatarajiwa kufanyika katika Hoteli ya Naura Springs iliyopo Arusha.

Mashindano hayo yanahusisha wanamitindo 16 wa kike na kiume kutoka Dar es Salaam na Arusha.

“Washiriki hao 16 wote watatambuliwa kutokana na hifadhi za taifa zilizopo na nia kubwa ni kuhakikisha tunatangaza vivutio vyetu kupitia sanaa,” alisema Sam.

Aliwataja wanamitindo kutoka Dar es Salaam na hifadhi watakazowakilisha kwenye mabano kuwa ni Consolatha Shimba (Tarangire), Willice Donard (Ruaha/Saanane), Amina Athumani (Mikumi) na Irene Hermes (Ngorongoro).

Wengine ni Emmanuel Shaxy (Mlima Kilimanjaro), Dismack Daxx (Kitulo), Abdallah Ally (Saadani), Alphasad Boniphace (Rubondo) na Haruna Hussein (Mkomazi).

Kwa upande wa wanamitindo wa Arusha watakaoshiriki shindano hilo ni Happness Wiliam (Udzungwa), Janeth Alex (Arusha), Glory Steven (Serengeti), Hope Sylvester (Mahale), Doris Michael (Ziwa Manyara), Shabani Jumanne (Katavi) na Saimon Mlokha (Gombe).

Alisema, baada ya ufunguzi washiriki watatembelea vivutio mbalimbali kuhamasisha utalii wa ndani na kupiga vita vitendo vya ujangili.

Fainali za mashindano hayo zitafanyika Oktoba jijini na mshindi atapata nafasi ya kutembelea Marekani, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza kutangaza vivutio vya utalii kupitia maonesho ya mavazi ya kimataifa.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwandago, Faustine Mwandago, ambao pia ni wadhamini wa shindano hilo alisema kampuni yake imejizatiti kuhakikisha kuwa mashindano ya mwaka huu yatakuwa ya aina yake na yenye mvuto kwa Watanzania.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi