loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wengi wataja manufaa ya kitambulisho cha kura

Katika uchunguzi wa haraka uliofanywa na HabariLeo kwenye vituo hivyo, ilibainika kuwa watu wengi wanajitoa kupata vitambulisho hivyo, si kwa kupiga kura pekee, bali kwa ajili ya kuvitumia katika huduma zingine kutokana na kukubalika na mamlaka kadhaa.

Taasisi kadhaa zikiwemo zile za fedha, zimekuwa zikikiamini na kukitambua kitambulisho cha mpiga kura kuliko kitambulisho cha taifa, kutokana na kitambulisho hicho cha mpigakura kuwa na saini.

“Nimepanga foleni tangu asubuhi na nataka niondoke nikiwa nimepata kitambulisho, lakini sina uhakika kama nitakitumia kwa ajili ya kupiga kura, ila najua nitatumia katika huduma zingine ambazo wanazikubali,” alisema Hamis Kassim, mkazi wa Mbagala.

Kauli hiyo inaungwa mkono na Mtendaji wa Butiama, Mtoni Kijichi, Magafu Michael aliyesema: “ Tumekuwa tunazidiwa na watu kwani wengi wanaochukua wanaonekana hawatatumia kupiga kura, naamini kama leo Serikali ikatoa tamko ya kutambua kitambulisho cha taifa katika huduma zingine, basi watu wasingekuwa hivi.”

Katika kituo cha mtaa wa Tupendane, Manzese, kulikuwa na watu wengi waliojitokeza, huku ofisa wa Tume ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake, alisema wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha wanawaandikisha watu wengi kwa siku pamoja na kufanya kazi katika mazingira magumu.

“ Tumekuwa tukiongeza idadi ya kuwaandikisha wananchi hadi kufika 100 kwa mashine moja, tumekuwa tukifanya kazi kwenye mazingira magumu, chumba kina joto ambalo linafanya mashine kushindwa kufanya kazi. “ Pia wananchi wengi wamekuwa hawana uelewa hivyo kujikuta wakilaumu. Kwa kawaida tunaweza kuchukua dakika tano, lakini kwa mzee dakika 20 muda ambao ningeweza kuandikisha watu wanne hivyo wananchi wanaishia kulalamika,” alisema.

Katika shule ya Mianzini, Mburahati yenye vituo 11 vyenye mashine 19 za kuandikisha, bado kulikuwa na misururu mirefu ya wananchi huku watendaji wakilalamikia wananchi kutoka maeneo mengine kwenda eneo hilo kujiandikisha.

Wakala wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Jackson Julius alisema, “Kazi ya uandikishaji inaendelea, ingawa idadi ya watu wanaojitokeza inazidi kuongezeka, lakini tumegundua kuwa kuna watu ambao maeneo yao wanashindwa kuandikishwa wanakuja hapa. Taratibu haziruhusu kumuandikisha mtu wa eneo lingine kwa madai kuwa ataruhusiwa kupiga kura ya rais pekee, mtu huyo ukimkatalia na kwa vile anakuwa amepanga foleni muda mrefu anaishia kulalamika.”

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Annastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi