loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wenye maduka Kariakoo wagoma

Mashine hizo ni muhimu kurahisisha kutunza kumbukumbu za kibiashara na zinasaidia kupunguza ama kuondoa misuguano wakati wa ukokotoaji wa kodi na kuongeza uwazi kwa mfanyabiashara.

Mgomo wa wafanyabiashara hao uliyakumba maduka mbalimbali yanayouza bidhaa za nguo, simu, mabegi, viatu, urembo wa wanawake, vyombo vya ndani na hata maduka ya vifaa vya ujenzi hali iliyosababisha wateja wengi wa ndani na nje ya nchi kulalamika.

Akizungumza na gazeti hili, mmiliki wa duka la simu katika Mtaa wa Msimbazi, Fadhil Anafs alisema sababu kubwa ya kufungwa kwa maduka hayo ni mashine za EFDs alizodai ni kero kubwa kwao na bei ni kubwa.

“Serikali ikitaka hizo mashine zifanye kazi kama inavyotakiwa jambo la muhimu ni kuwashirikisha wafanyabiashara wao watoe muundo utakaokuwa rahisi kwa mashine hizo kufanikiwa,” alisema Anafs.

Naye Yassin Rajab, mfanyabiashara wa Mtaa wa Kongo alisema kinachowakera ni namna TRA inavyowakadiria bidhaa walizonazo kitu ambacho katika uhalisia hakipo hivyo.

Akizungumza na vyombo vya habari juzi kuhusu uhakiki wa mashine hizo, Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade alisema uhakiki umebaini wafanyabiashara walengwa kutonunua mashine hizo, wengine wanakuwa nazo lakini hawazitumii na wengine kuwaibia wananchi kwa kutoa risiti za mashine zisizosajiliwa TRA au kutambulika na mamlaka hiyo.

RAIS John Pombe Magufuli anaongoza kwenye ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi