loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Wenye ulemavu hupewa matibabu bure’

Mbunge huyo alitaka kufahamu mikakati ya Serikali katika kupunguza au kuondoa tatizo la kuhangaika kwa walemavu wanaomba misaada ya kiafya wanapougua.

Pia mbunge huyo alitaka kujua ni walemavu wangapi mpaka sasa wameshapewa matibabu ya bure au kusomeshwa na kupatiwa ajira kwa wale wenye vigezo vinavyotakiwa.

Akifafanua zaidi wakati akijibu maswali hayo, Dk Mwinyi alisema kupitia Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Huduma kwa Watu wenye Ulemavu ya 2004, Serikali inatekeleza mipango mbalimbali kwa watu wenye ulemavu.

Alisema mipango hiyo ni pamoja na utoaji wa haki na ulinzi kwa watu wenye ulemavu katika masuala ya elimu, ajira na mafunzo ya ufundi na pia watu wenye ulemavu wasiojiweza kabisa na wasio na ndugu, hutunzwa katika makazi ya watu wenye ulemavu na wasiojiweza.

Dk Mwinyi alisema pia Sera ya Afya inawatambua watoto, wajawazito, magonjwa ya kusendeka na wazee, pia utaratibu unatambua watu wasio na uwezo ukiwajumuisha watu wote wakiwemo walemavu.

Alisema Serikali haina mfumo wa kupata takwimu za kitaifa, lakini imeweka mazingira ya kumwezesha mtu mwenye ulemavu kupata elimu jumuishi kwenye shule na vyuo bila ubaguzi.

Dk Mwinyi alisema zipo shule na vyuo maalumu kwa watu wenye ulemavu, kwa wale ambao hawawezi kupata elimu jumuishi ambapo kwa sasa kuna wanfunzi 94 wenye ulemavu walio katika Chuo cha Marekebisho kwa Watu enye Ulemavu cha Yombo na Chuo cha Wanawake Wasioona Singida kuna walemavu 19.

Alisema kwa kuzingatia sheria ya watu wenye ulemavu kila mwajiri anatakiwa kuajiri asilimia tatu ya watu wenye ulemavu. Waziri huyo alisema sasa Serikali ina jumla ya watumishi 500,028 miongoni mwao 2,025 ni watu wenye ulemavu sawa na asilimia 0.4.

Alisema Wizara itaendelea kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo ili kuona watu wenye ulemavu wanapata huduma za elimu, ajira na afya sawa na watu wengine.

RAIS John Magufuli amesema Manispaa ya Ilala imepandishwa ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi