loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wenye uwezo wasaidieni wajasiriamali'

Katibu wa Chama cha Wajasiriamali Wadogo kutoka katika Kata ya Bulyanhulu (BECOS), Mwita Bhoke aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na gazeti hili muda mfupi baada ya kufanya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kutunisha mfuko wa chama hicho.

Bhoke alisema kuwa lengo la kuchangia harambee hiyo ni kutunisha mfuko wa chama hicho kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuweza kuanzisha ushirika ambao ungeweza kuwasaidia wajasiriamali wadogo katika Kata ya Bulyanhulu.

Alisema kuwa chama hicho kinakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na mtaji pamoja na masoko ya bidhaa na huduma katika jitihada za kujikwamua katika umasikini uliopo kwa wajasiriamali wanachama.

Katibu huyo alisema chama hicho kilichoanzishwa mwaka huu kimekuwa katika wakati mgumu kwa kufanya shughuli za ujasiriamali usio na manufaa makubwa kutokana na kutokuwa na mtaji wa kutosha, mafunzo, zana bora na masoko.

Alisema katika Kataya Bulyanhulu kihistoria kuna shughuli za uchimbaji mdogo wa dhahabu unaoendelea tangu miaka ya 1990 huku ongezeko kubwa la watu likikadiriwa kuwa ni jumla ya watu 50,000 kwa vijiji sita, hatua ambayo itawasaidia kujikomboa endapo watapata mtaji wa kuendesha biashara.

Katika harambee hiyo iliyokuwa na lengo la kuchangia kiasi cha Sh milioni 20, jumla ya Sh milioni 16 zilichangishwa zikiwa ni ahadi mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara na kampuni zilizopo mjini Kahama.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la ...

foto
Mwandishi: Raymond Mihayo, Kahama

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi