loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wizara kuboresha kilimo

Alisema hatua hiyo imelenga kuwawezesha vijana wengi wa mijini na vijijini washiriki kwenye sekta ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara ambacho kitaboresha hali zao za kiuchumi na kukuza pato la taifa.

Chiza alisema hayo kwenye hotuba yake ya siku maalumu ya BRN kwa wizara hiyo iliyofanyika jana kwenye eneo la skimu ya umwagiliaji katika Kijiji cha Mkindo, wilayani Mvomero, mkoani hapa.

Alisema, kwa sasa sekta ya kilimo inachangia kwa asilimia 24.5 ya pato la Taifa na inachangia kwa zaidi ya asilimia 100 ya mahitaji cha chakula nchini, inatoa ajira kwa wastani wa asilimia 74 ya Watanzania huku ikichangia kwa asilimia 33 ya fedha za kigeni.

Hata hivyo alisema, kulingana na takwimu ya sensa ya Taifa ya mwaka 2012, Watanzania wamefikia zaidi ya milioni 45 ambapo kati ya hao, asilimia 15.1 ni vijana na wengi hawana ajira.

Alisema ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, wizara yake kupitia mfumo wa BRN imeweka mkakati endelevu utakaojenga mazingira bora na rafiki yatakayowavutia vijana wengi kushiriki kwenye kilimo cha mazao ya chakula na biashara.

Chiza alisema, mpango huo umelenga kukabiliana na changamoto mbalimbali na umeweka vipaumbele katika mazao ya mpunga, mahindi na miwa kama mazao ya kimkakati katika usalama wa chakula ili kuongeza uzalishaji wake kwa matumizi ya nchini na ziada kuuzwa nje.

Kuhusu mpango wa ruzuku ya pembejeo, Waziri Chiza alisema ulipoanza hali ya chakula nchini ilikuwa ni asilimia 88 jambo lililoilazimu Serikali kuagiza chakula nje ili kujazia upungufu. Hata hivyo, alisema kwa miaka mitatu iliyopita, taifa limejitosheleza kwa chakula kwa zaidi ya asilimia 100 na mwaka 2013/14 utoshelevu ni asilimia 118.

ASKOFU mpya wa Jimbo Katoliki Mpanda, Eusebius Nzigilwa amekumbushwa kuwa ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi