loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga, Azam kambini mechi za Afrika 2014

Azam FC imeingia kambini kujiandaa kwa mechi ya kwanza ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Ferroviario de Beira ya Msumbiji itakayopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Jumapili wiki hii.

Meneja wa Azam FC, Jemadari Said alisema wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja baada ya mechi ya Jumapili na jana walianza rasmi mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo.

“Jana (juzi) tulipumzika, lakini leo (jana) tumeanza mazoezi rasmi kwa ajili ya Kombe la Shirikisho mchezo ambao tutaanza nyumbani,” alisema Jemadari.

Msimu uliopita, Azam FC pia waliiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo baada ya kumaliza ligi katika nafasi ya pili, na wakiitoa Ferroviario watacheza na mshindi kati ya St Michel ya Shelisheli na ASSM Elgeco Plus ya Madagacar.

Kwa upande wake, Yanga ambao ni mabingwa wa Tanzania Bara, wameingia kambini jana asubuhi kujiandaa na mechi ya michuano ya awali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Komorozine de Domon ya Comoro itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Jumamosi wiki hii.

Katika hatua nyingine, Komorozine inatarajiwa kutua Dar es Salaam leo saa 10 jioni tayari kwa mechi hiyo.

KLABU ya Chelsea imemtangaza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi