loader
Picha

Yanga kucheza Kagame kimtindo

Yanga iliyopo Kundi A, itafungua dimba Ijumaa ijayo kwa kupambana na wenyeji Rayon Sport kabla ya mchezo wa pili, dhidi ya Atlabar ya Sudan Kusini na itamaliza na ndugu zao, KMKM ya Zanzibar.

Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo aliyasema hayo jana baada ya mazoezi ya asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Mabibo Dar es Salaam.

Maximo alisema lengo la kufanya hivyo ni kutaka kutumia muda mwingi kuiandaa timu kubwa ili ifanye vizuri kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

“Nataka nipate muda wa kutosha kukiandaa kikosi imara ambacho kitajumuisha na wachezaji waliopo kwenye timu za taifa kule Pemba,” alisema Maximo na kuongeza: “Lakini watu wasidhani kuwa tumedharau mashindano ya Kagame, tuna kikosi bora cha vijana ambacho tumekuwa tukifanya nacho mazoezi kila siku, nina imani kubwa kitatuwakilisha vizuri.”

Maximo alisema timu hiyo ya vijana itakuwa chini ya kocha Leonard Neiva pamoja na msaidizi wake, Shadrack Nsajigwa, wakati timu ya wakubwa itakayokuwa Pemba kwa kambi ya wiki mbili ikijiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii na Ligi Kuu itakuwa chini yake na msaidizi Salvatoy Edward.

“Kuna wachezaji sijawaona, zaidi ya kusikia sifa zao kutoka kwa watu na wengine nimewahi kufanya nao kazi nikiwa kocha wa Taifa Stars kama Mrisho Ngasa, Nadir Haroub ‘Cannavaro, Kelvin Yondani na wengine kutoka Rwanda na Uganda, sijui uwezo wao. “Ndiyo sababu ya kutaka nipate muda mzuri wa kuwaona ili kupata timu imara itakayoshiriki ligi na kutwaa ubingwa ili kuiweka Yanga juu,” alitamba.

Kocha huyo raia wa Brazil, alisema wakiwa Pemba, Yanga itacheza mechi mbili za kirafiki kabla ya kurudi Dar es Salaam ambako itaungana na timu ya vijana itakayokuwa imerudi Kagame na watachagua wachezaji wachache kujiunga na timu ya wakubwa.

“Baada ya hapo tutaingia kambini na tutacheza mechi tatu za kirafiki kisha tutapambana na Azam FC kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Baada ya hapo timu itakuwa ipo tayari kwa ajili ya kuanza kwa ligi tukiwa na matumaini ya kurudisha taji msimu ujao,” alisema Maximo mwenye mkataba wa miaka miwili.

Maximo alisema kwa ratiba hiyo, ana uhakika timu yake itanyakua ubingwa wa Tanzania Bara kulingana na wachezaji aliokuwa nao pamoja na ushindani uliopo kwa wachezaji wakongwe na vijana ambao wamekuwa wakibadilika kila siku.

BAADHI ya makocha na wachambuzi wa soka nchini ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi