loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga kuiburuza TFF mahakamani

Hivi karibuni TFF ilisema imepokea amri ya Mahakama Kuu (Kitengo cha Kazi) kukamata Sh milioni 106 za Yanga kutokana na mapato ya mlangoni kwenye mechi zake ili kuwalipa waliokuwa wachezaji wake Stephen Malashi na Wisdom Ndlovu, agizo ambalo TFF imeshaanza kulitekeleza.

Wachezaji hao waliingia mkataba na Yanga mwaka 2010, lakini Yanga ilivunja mikataba yao na hivyo kuamua kufungua kesi mahakamani kupinga suala hilo na kutaka walipwe haki zao ambapo mahakama ikaamuru walipwe Sh milioni 106.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na kusainiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, sheria ya usajili wa wadhamini Cap. 318 na kanuni za kesi za madai zote zinatakiwa kuwa kama mali zozote zilizo chini ya wadhamini hivyo wanatakiwa kuuhusishwa katika mchakato wa kesi hiyo.

“Wafaidika hawawezi kwa mujibu wa sheria kushtakiwa mahakamani wakati wao ni wafaidika tu wa mali zilizo chini ya udhamini,” ilisema taarifa hiyo.

Pia, ilisema wadhamini hao wamewapa maelekezo mawakili kufanya maombi yanayohitajika kwa Majaji wa Mahakama ya Kazi kuomba marejeo ya mwenendo wa kesi na namna gani sheria iliweza kupindishwa katika Baraza la Usuluhishi na Uamuzi na kuona hatua gani za kurekebisha hali hiyo zinaweza kuchukuliwa.

Taarifa hiyo ilisema wachezaji wote wawili ni watu wasio na makazi ya kudumu na kwamba mmojawao ameshawahi kulipwa kupitia TFF na haijawahi kutiliwa maanani na kuongeza: “Yanga inaamini Jaji wa Mahakama Kuu akiongozwa vizuri atatoa nafuu stahiki”.

Taarifa hiyo ilisema, wameamua kupeleka malalamiko yao kwa Jaji Mkuu wa Tanzania ili kuona kama utaratibu wa kiutawala ulifuatwa na kutekelezwa kwa usahihi pamoja na kutokuwepo kwa faili la Mahakama ambalo lilikuwa tayari katika Mahakama ya Rufaa kutokana na kuwepo kwa maombi mawili namba 163 ya mwaka 2013 na 165 ya mwaka huo.

Ilisema wakati maombi namba 163 yalifutwa mwaka huo, mengine hayajaitwa kwa ajili ya kusikilizwa au kufutwa. Taarifa hiyo ilifafanua, wadhamini ndio wamiliki wa mali zote za Yanga bila kujali kuwa zisizohamishika, zinazohamishika au fedha hivyo kuhoji ni kwa namna gani TFF inaruhusu utekelezaji wa amri dhidi ya klabu na si wadhamini.

“Sisi tunathubutu kusema kwamba TFF ilipaswa kuijibu Amri ya Mahakama kwamba wao hawana fedha ya klabu ambao ni wafaidika,” alisema. “Hatua ya kuruhusu fedha za wadhamini kushikiliwa ni kinyume cha sheria hivyo tunaitaka irudishe fedha hizo pamoja na riba yake au itufikishe mbele ya vyombo vya sheria kwa matumizi mabaya ya fedha za wadhamini."

TIMU ya soka ya Polisi Zanzibar inayoshiriki Ligi Kuu ya ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi