loader
Dstv Habarileo  Mobile
Yanga kuwachuja ‘maproo’ wa Mzungu

Yanga kuwachuja ‘maproo’ wa Mzungu

Awali, Yanga walisema watashirikiana na kocha huyo katika kuwapata wachezaji wazuri watakaoisaidia kuchukua ubingwa msimu ujao na pia kushirikiana naye kumpata mwingine.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu alisema wachezaji walioahidiwa na kocha hawajafika, kwani walitakiwa kumuaga jana jioni kisha aende Ghana kumitiza ahadi ya wachezaji.

“Kocha alienda Dubai kwa hivyo bado hajaleta wale wachezaji, tulikuwa tunazungumza naye kwanza, baada ya kumuaga tutaachana naye rasmi, kisha atarudi Ghana na ikiwa atapata hao wachezaji na kuwapendekeza, tutawaangalia,” alisema Njovu.

Alisema kuna wachezaji wanaweza kupendekezwa, lakini wakawa ni gharama zaidi, na kuongeza kuwa sio lazima kwa mchezaji atakayeletwa achukuliwe kuichezea Yanga.

Kuhusu wachezaji wa kigeni waliopendekezwa na klabu nyingine wawe watano, alisema wanakubaliana nalo, na kwamba kama
itapitishwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) basi kwa vile wanao wanne, huenda akaongeza mmoja.

Wachezaji wa kigeni waliopo sasa ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi. Katika hatua nyingine, Njovu
alisema marekebisho ya kipengele kimoja kwenye Katiba yao, hakiwezi kuzuia mchakato wa uchaguzi kuendelea.

Hivi karibuni, TFF ilirudisha Katiba hiyo mikononi mwa Yanga kwa ajili ya kuingiza kipengele cha Kamati ya Maadili ambacho awali hakikuwepo ambapo Yanga walisema watakipitisha katika Mkutano Mkuu wa wanachama utakaofanyika Juni mosi mwaka huu.

Alisema kwenye mkutano wa wanachama watakwenda kupitisha agizo hilo, kwani wakikataa hawawezi kufanya uchaguzi kwa vile
hawataruhusiwa na TFF.

Njovu alisema Uchaguzi Mkuu utafanyika Juni 15, mwaka huu kama ilivyopangwa, na kwamba baada ya marekebisho ya kipengele  hicho kitakachobaki ni kupitishwa TFF na kwa Msajili hivyo, ana imani haitochukua muda mrefu.

Kabla ya mwaka huu, kufanya marekebisho ya Katiba hiyo, pia waliwahi kurekebisha tena mwaka 2010.

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi