loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Yanga yaenda Comoro bila Kaseja, Tegete

Wachezaji hao wameachwa kutokana na sababu mbalimbali ambapo Kaseja anaumwa ugonjwa wa malaria, wakati Tegete anamuuguza mama yake.

Alisema Tegete alilazimika kuondoka katika kambi hiyo na kuwahi mkoani Mwanza kumuuguza mama yake na kwa sasa anaendelea vema.

“Kama ambavyo unaweza kuwa umeona kwa sasa hatupo naye katika mazoezi yetu ambayo tumefanya leo (jana) hapa Karume,”alisema kocha msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwasa.

Akizungumzia Kaseja, alisema alianza kuumwa malaria jana na hivyo kulazimika kuachwa katika kikosi hicho. Hata hivyo, Mkwasa alisema kuwa kikosi chake kipo katika hali nzuri kimchezo na kukosekana kwa wachezaji hao hakutaathiri ushindi wa timu hiyo.

Alisema kuwa wachezaji wote wapo katika hali nzuri kimchezo na kuongeza ana uhakika wa kupata ushindi mkubwa dhidi ya timu hiyo.

Aliongeza kuwa Yanga inatambua umuhimu wa mchezo huo katika michuano hiyo na ina uhakika matokeo yatakuwa mazuri.

Katika kuonesha maandalizi mazuri katika mchezo huo utakaofanyika katika mji wa Moroni, Mkwasa alisema kuwa timu hiyo iliamua kuhamishia kambi yake Karume ili kufanya mazoezi kwenye uwanja wa nyasi za bandia kwa kuwa mchezo wao wa Comoro utafanyikia kwenye nyasi kama hizo.

“Maandalizi ni mazuri sana na kwa sasa tunamalizia yale ya mwisho kamili kabisa kwenda kufanya mashambulizi na uhakika ni kwamba tutawapiga zaidi ya zile saba,” alisema Mkwasa.

Yanga ambayo imeanza kwa mkwara wa kupata ushindi wa kishindo wa mabao 7-0, ikivuka hatua hiyo itakutana na Al Ahly ya Misri. Mchezo huo utaanzia hapa jijini Dar es Salaam, Februari 29 mwaka huu na marudiano ni Machi 9 jijini Cairo, Misri.

MSANII wa Kizazi Kipya, Beka Flavour ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi