loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga yaiendea Al Ahly mafichoni

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto alisema kikosi cha Yanga chenye wachezaji 25 pamoja na benchi la ufundi kilianza mazoezi juzi jioni katika Uwanja wa Kaunda makao makuu ya klabu hiyo, mtaa wa Twiga na Jangwani.

“Wachezaji wote wapo katika hali nzuri, mpaka sasa hakuna mchezaji majeruhi kuelekea mchezo huo,” alisema Kizuguto.

Alisema kocha anatambua mchezo huo utakuwa mgumu, kwani Al Ahly wana uzoefu na michezo ya kimataifa lakini na wao wana malengo na zaidi ni kufanya mapinduzi kwa kushinda.

“Kwa vile kocha anawafahamu Al Ahly vizuri hakuna kitakachoshindikana kwa sababu tayari tumepata mbinu zao kutoka kwa kocha msaidizi Boniface Mkwasa, kilichobaki ni kuwaandaa wachezaji kiakili,” alisema.

Aidha, katika mchezo huo mshambuliaji wa Kimataifa, Emmanuel Okwi atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaoshuka dimbani kwani tayari leseni yake ya michuano ya CAF imeshawasili na Kizuguto amelithibitisha hilo kwa waandishi wa habari jana.

Wakati huo huo, Kizuguto alisema timu ya Al Ahly inatarajiwa kuwasili leo alfajiri saa 12 na moja kwa moja watafikia katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro ambapo ndio itakuwa kambi yao kuelekea mchezo wa Jumamosi.

Alisema, kikosi hicho kinatarajiwa kuwasili na msafara wa watu 35 wakiwemo wachezaji 22, benchi la ufundi wanane pamoja na viongozi watano.

Leo na kesho jioni kikosi cha Ahly kitafanya mazoezi kwenye Uwanja wa IST uliopo Upanga, na Ijumaa jioni watapata fursa ya kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo huo.

Alisema tiketi zitaanza kuuzwa kwenye vituo mbalimbali kuanzia Ijumaa ambapo kiingilio cha juu ni Sh 35,000, Sh 25,000, Sh 13,000 na cha chini ni Sh 7,000.

Rekodi ya Al Ahly: Wana mataji 19 moja zaidi ya mataji 18 ya AC Milan, imeshinda mara nane kombe la mabingwa barani Afrika, mwaka 1982,1987, 2001, 2005, 2006, 2008, 2012, na 2013.

Makombe manne ni ubingwa wa Kombe la washindi 1984,1985,1986, 1993. Mara sita imetwaa Kombe la CAF, Super Cup 2002, 2006, 2007, 2009, 2013, na 2014 na moja likiwa la Afro-Asian Cup mwaka 1988.

VINARA wa Ligi Kuu soka Tanzania, Azam FC ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi