loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yassin aombwa kuendelea na michuano ya Muungano

Yasin amekuwa akiandaa michuano ya Muungano tangu mwaka 1996 na hivi karibuni alitangaza kuacha kufanya hivyo, lengo likiwa kuwapisha wadau wengine wa michezo kutoa mchango wao.

CCM walitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari mjini Mafinga, baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mufindi kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akitangaza maazimio ya kikao hicho cha ngazi ya juu cha CCM wilayani Mufindi, Katibu wa CCM wilayani Mufindi, Miraji Mtaturu alisema CCM inamtaka Yassin aendelee kuratibu mashindano hayo muhimu.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mufindi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi