loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yassin Ustaadh aula kimataifa

Akizungumza Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa ECAPBA, Boniface Wambura alisema Ustaadh wa Tanzania ameteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa ECAPBA.

Ustaadh amejaza nafasi ya Celestino Mindra wa Uganda aliyekuwa Rais wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa ya Uganda (UPBC) wakati Simon Kategole wa Uganda ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa ECAPBA kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Shaban Ogolla wa Kenya ambaye yuko masomoni Marekani. Daudi Chikwanje wa Malawi anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa ECAPBA.

Wambura alisema pia Nelson Sapi wa Zambia ameteuliwa kuwa Naibu Mweka Hazina wa ECAPBA akimsaidia Nemes Kavishe wa Tanzania na yeye (Wambura), anabaki kuwa Ofisa Habari wakati wajumbe wanne wameongezwa kwenye Kamati ya Utendaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Malawi na Ethiopia pamoja na Roman Chuwa wa Jiji la Arusha.

Aidha, shirikisho hilo la ngumi limemshukuru Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo kwa kukubali kuwa mlezi wake na kuipatia ofisi katika Manispaa ya jiji la Arusha ikikumbukwa kwamba ndicho chombo cha kuwaunganisha vijana cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Katika malengo yake, ECAPBA itafanya kazi kwa karibu na EAC ili iwe chachu ya utekelezaji wa maamuzi ya Jumuiya katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati.

Pia Wambura alisema ECAPBA itafanyia utekelezaji maamuzi yote yanayohusu maendeleo ya vijana pamoja na ushirikiano wa utamaduni na michezo wa EAC kama yaliyopendekezwa na jumuiya hiyo, ikiwa ni pamoja na kutengeneza ajira kwa vijana wa Afrika Mashariki na Kati.

wakati huohuo OGANAIZESHENI ya Ngumi cha Kulipwa (TPBO) imeandaa mkutano wa wadau utakaofanyika Februari mosi, mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Vijana Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo ambao utawakutanisha mapromota, waamuzi, makocha na mabondia, utaanza saa 3:30 asubuhi na utakuwa ukijadili mwenendo wa ngumi za kulipwa, kuelimishana juu ya sheria za kulipwa pamoja na kufahamiana.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa TPBO, Yassin Abdallah alisema lengo la mkutano huo ni kujenga ushirikiano kati ya wadau ili kujenga ushirikiano na kuelimishana juu ya mambo yanayowahusu.

“TPBO ikiwa na ushirikiano itakuwa rahisi kupata udhamini, vilevile sheria nyingi za ngumi zimebadilika hivyo tunataka wadau wajue mabadiliko hayo ili kuboresha na kuondoa malalamiko ambayo hayana msingi,” alisema Abdallah.

Mkutano huo chini ya ufadhili wa Kampuni ya Kitwe Traders, utakuwa wa kwanza kuwakutanisha wadau wote wa ngumi nchini. Pia TPBO imewaalika viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), na viongozi wengine wote wa ngumi za kulipwa watakuwepo kama vile Emmanuel Mlundwa, Nemes Kavishe, Onesmo Ngowi, Abdallah Kinyogoli, Rashid Matumla, Zuwena Kibena ili kujenga ndondi nchini.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi