loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Zantel yakanusha hisa zake kununuliwa Tigo, Vodacom

Jumatano wiki hii, gazeti moja la kiingereza la kila siku liliripoti kuwa kampuni ya Etisalat kwa kushirikiana na Deutsche Bank AG inaangalia uwezekano wa kuuza hisa zake asilimia 65, hatua ambayo imezivutia Vodacom Group Ltd na Millicom International Cellular.

“Hizi ni taarifa za magazeti tu,” Mwenyekiti Al Haddad aliwaambia waandishi wa habari jana wakati akifungua duka jipya la Zantel lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.

Alisema Etisalat Group ambayo ilikuwa na hisa ya asilimia 65 ilitangaza hivi karibuni kuongeza hisa zake Zantel kufikia asilimia 85. Asilimia nyingine 15 zinamilikiwa na serikali ya Zanzibar.

Alipoulizwa kama kuna mpango wa Etisalat kununua hisa asilimia 15 zilizobaki, Mwenyekiti huyo alisema kampuni hiyo inaheshimu uwepo wa wadau wazalendo.

Akizungumzia uzinduzi wa duka hilo jipya, Al Haddad alisema huo ni mwanzo mpya wa kufungua maduka kama hayo nchini nzima.

Naye, Mkurugenzi wa wateja wakubwa wa Zantel, Ahmed Seif Mohamed alitoa ahadi ya kuimarisha huduma zao nchi nzima. Katika miaka ya hivi karibuni, Zantel imekuwa ikifanya mapinduzi makubwa katika sekta ya simu za mkononi Tanzania kwa ubunifu ambao umekuwa ukisaidia kustawisha maisha ya watu.

Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na Z-Kilimo ambayo huwezesha wakulima hata wa vijijini kuweza kupata taarifa muhimu za jinsi ya kuongeza uzalishaji na hivyo kuendeleza sekta ya kilimo.

Huduma nyingine ni Islamic Portal, Discover Tanzania (Tourist Portal) na Reverse Ring Back tone (RRBT) ambazo zinawasaidia Watanzania kwa namna mbalimbali. Pia Zantel ni moja ya kampuni za simu za mkononi nchini zilizofikia makubaliano na kampuni nyingine za simu kuwezesha wateja wao kutuma na kupokea pesa miongoni mwao.

Hii ni huduma ya kwanza ya aina hiyo Afrika ambapo mteja wa kampuni hiyo wa huduma ya EzyPesa anaweza kutuma na kupokea pesa kwenda mitandao mingine.

Kwa sababu ya juhudi zake katika kuokoa maisha ya mama na mtoto, Zantel imeshawahi kupata tuzo inayoheshimika ya GSMA kwa mradi wa “Mobile Baby”, wakati mkakati wa “Fight Against Malaria” ulitambulika na Wizara ya Afya.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi