loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Zanzibar, Comoro kushirikiana kukuza utalii

Alisema ushirikiano huo utakuza sekta hiyo kwa manufaa ya serikali na wananchi wa pande mbili hizo.

Dk Shein alisema hayo, alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa mwandishi wa Kituo cha Taifa cha Televisheni na Redio Comoro jana katika fukwe ya Mitsamihouli katika siku yake ya pili ya ziara yake ya siku nne.

Alisema Comoro ina nafasi nzuri ya kuendeleza sekta ya utalii, kama ilivyofanya Zanzibar.

Akieleza kituo hicho kuwa eneo hilo la Mitsamihouli linafanana na maeneo mengi ya Zanzibar kama vile Nungwi, Kiwenga, Kizimkazi na mengineyo, ambayo yanatumika kwa shughuli za kitalii.

Alisema Serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuvutia wawekezaji na kuchukua hatua nyingine kuimarisha sekta hiyo.

Alifafanua kuwa sekta hiyo ni moja ya maeneo yanayopewa kipaumbele katika mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano kati ya Zanzibar na Comoro, yanayoendelea hivi sasa wakati wa ziara yake.

Dk Shein alibainisha kuwa mbali ya ushirikiano baina ya pande mbili hizo, Mpango wa Magharibi wa Bahari ya Hindi wa Changamoto za Ukanda wa Pwani ambao ulizinduliwa hivi karibuni nchini Samoa, ambapo Zanzibar na Comoro ni washiriki, utatoa fursa zaidi kwao kushirikiana, kwani moja ya malengo yake ni kuimarisha sekta ya utalii miongoni mwa washiriki wa mpango huo. Dk Shein anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku nne leo.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Said Ameir, Moroni, Comoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi