loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Zanzibar kufanya sensa ya walemavu

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Alhabib Fereji wakati alipozungumza na walemavu huko Wete katika ziara ya kuangalia miradi ya walemavu.

Alisema Serikali hadi sasa haijui idadi kamili ya walemavu waliopo nchini pamoja na aina ya ulemavu wao, hatua ambayo inarudisha nyuma juhudi za kuwaondolea matatizo waliyonayo.

“Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ambayo inashughulikia moja kwa moja masuala ya walemavu inakusudia kufanya sensa ambayo itawawezesha kujua idadi kamili ya walemavu wote waliopo nchini,” alisema.

Alisema Serikali ipo katika mchakato wa kuangalia jinsi ya kuwawezesha walemavu kupiga hatua ya maendeleo na kuondokana na tatizo la kuwa omba omba.

Kwa mfano alisema katika sekta ya Elimu, Serikali imepiga hatua kubwa kwa kuanzisha elimu ya mjumuisho kwa mahitaji maalumu kwa watu wenye matatizo ya ulemavu wa aina mbalimbali ikiwemo wasioona.

Akifafanua zaidi alisema mafanikio makubwa yamepatikana katika eneo hilo ikiwemo kuwepo kwa walemavu waliohitimu masomo yao ya vyuo vikuu kutokana na fursa za masomo kwa kundi hilo.

‘”Kazi kubwa iliopo sasa ni kuimarishwa kwa elimu mjumuisho ambayo itawawezesha walemavu kuongeza ubora wa ufaulu wao kwa kiwango kikubwa, “alisema.

Mapema Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Mohd Ame alisema mara ya mwisho walifanya sensa katika mwaka 2000-2011 ambayo walipata idadi ya walemavu 6,400 waliopo Pemba.

Alisema walemavu waliopo Pemba ambao wanasoma katika shule zenye mahitaji maalumu wanahitaji kupatiwa vifaa mbali mbali vitakavyowasaidia kuweza kupiga hatua ya maendeleo katika sekta ya elimu.

MAFUNDI umeme nchini wametakiwa kufanya ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi