loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

ZFA yaaswa kuipa uzito Ligi ya Wanawake

Mwito huo umetolewa na kocha mkuu wa timu ya Kidimni Queens Ridhwan Amour alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na maendeleo ya ligi hiyo iliyoanza wiki iliyopita.

Alisema kuwa ligi yao ni ligi kama zilivyo ligi nyingine na wachezaji wanapoumia wanahitaji kupatiwa huduma ya kwanza lakini cha kushangaza toka kuanza kwa ligi hiyo bado hakujaletwa madaktari.

“Hii ni ligi kubwa ambayo inahitaji kupatiwa kila aina ya mahitaji ambayo yanatakiwa kuwepo sasa kama wachezaji wanacheza bila ya uwepo wa madaktari wanapoumia je itakuwaje,” alihoji.

Hata hivyo alisema kuwa amefurahia uamuzi wa chama hicho kuirejesha Ligi ya Wanawake na kusema kuwa ni njia mojawapo ya kupata wachezaji katika timu ya Taifa ya Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.

Alisema, hiyo ni fursa adhimu kwa wachezaji kujituma na kuonesha uwezo wao ili waweze kuchaguliwa kuunda timu za Taifa.

“Tumezoea kuona sura zile zile katika timu zetu lakini kwa utaratibu huu sasa tutajipa matumaini ya kupata wachezaji wengi,” alisema.

Hata hivyo alisema kuwa maboresho zaidi yanahitaji kufanywa ili kupata mvuto zaidi ligi hiyo. Jumla ya timu sita zinashiriki ligi hiyo ambayo inatarajiwa kufikia tamati yake Januari 26 mwaka huu.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi