loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ziara ya magwiji wa Real Madrid itufumbue macho

Magwiji hao wa zamani wameletwa nchini na Kampuni ya TSN Supermarket na leo wanatarajiwa kucheza na wachezaji wa zamani wa Tanzania, Tanzania All Stars kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mbali ya mchezo wa leo, magwiji hao watakwenda Arusha ambako watatembelea mbuga ya Taifa ya Ngorongoro na kisha kupanda Mlima Kilimanjaro. Kwa hakika hii ni ziara muhimu sana kwa Tanzania kwa wapenda michezo na Taifa kwa ujumla wake.

Kwa wapenzi wa soka, hakuna asiyeifahamu klabu ya Real Madrid licha ya kuwa iko mbali na taifa letu, lakini kwa sababu ya ubora wake wa soka, inafahamika kwa Watanzania wengi.

Ni miamba ya soka yenye makazi yake Madrid nchini Hispania na hivi karibuni, ilitwaa taji la 10 la Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikidhihirisha ubora wake katika mchezo wa soka duniani.

Kwa hiyo, ni timu yenye mafanikio makubwa duniani na ambayo siyo tu inawavutia mamilioni ya mashabiki duniani, lakini pia wanasoka wengi duniani wanajisikia ufahari kuichezea timu hiyo.

Hilo linathibitishwa na ugeni uliokuja nchini, kwani una wachezaji wa mataifa mbalimbali duniani, hivyo kuthibitisha ubora wake. Kwa hiyo, kwa Tanzania hii ni fursa kubwa kwa kuja kwa magwiji hao nchini kwani hii ni ziara ya kwanza kwao barani Afrika.

Ni bahati iliyoje kwetu. Si hivyo tu, kuja kwao ni fursa nyingine kwa Tanzania kutangaza utalii wake kwani licha ya kucheza mechi leo, lakini ziara yao kaskazini mwa Tanzania, itafungua fursa nyingine ya kutangazwa kwa vivutio vyetu vya utalii.

Kama alivyoeleza mmoja wa magwiji wao jana Dar es Salaam, Luis Figo, atarudi tena Tanzania kwa sababu amesikia mambo mengi mazuri kikiwamo kisiwa cha Zanzibar ambacho ameahidi kuja na familia yake kukitembelea.

Kwa hiyo, ni muhimu kwa mamlaka za michezo nchini pamoja na zile zinazohusika na utalii, kutumia ziara hii muhimu ya Real Madrid kutufumbua macho katika masuala ya michezo na utalii.

Katika michezo, tunaweza kuwatumia wachezaji hao wa zamani kujenga ushirikiano na klabu yao ya zamani Real Madrid, lakini pia na mashirikisho mbalimbali yakiwamo ya nchi zao.

Hawa wana ushawishi mkubwa katika nchi zao na katika soka duniani, hivyo hii ni fursa nzuri kuitumia kwa ajili ya kujenga ushirikiano utakaoisaidia Tanzania katika sekta hizi mbili muhimu za michezo na utalii.

Tunapowakaribisha magwiji hawa wa Real Madrid ni muhimu kutambua hilo na kutumia ziara yao kunufaika kama Taifa.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi