loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Zitto: Bunge lidhibiti watendaji serikalini

Taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, kuhusu madai ya kwamba kiasi cha Dola za Marekani milioni 250 zilizopaswa kuendelea kuwapo katika akaunti ya ‘Tegeta Escrow Account’ na sio kulipwa katika akaunti ya PAP.

Alidai kwamba watendaji wanatoa matamshi ya kuonyesha kwamba chombo hicho ni chombo cha watu wasiofaa na kwamba watu wanaofaa wanazungumza nje ya Bunge.

Zitto alisema watendaji wa aina hiyo kama wana ushahidi wa rushwa dhidi ya mbunge ama yeyote hawapaswi kupayuka ovyo; bali kwa nafasi zao wanaweza kuwasiliana na vyombo vya dola kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na polisi ili kuchunguza na kuchukua hatua.

Alisema ipo haja ya kufumbua macho kuona na kuondoa hisia binafsi zenye kubebwa na itikadi, chuki na misimamo ya kisiasa na kuwa wazalendo katika kusimamia utaifa.

Zitto alisema inatarajiwa kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), atafichua ukweli wa suala hilo na TAKUKURU iwafikishe mahakamani wahusika bila kujali nyadhifa zao serikalini.

Kadhalika alisema uchunguzi huo ni muhimu ukawalenga vigogo na wanasiasa wakubwa wakiwamo watendaji waandamizi

WASHEREHESHAJI katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe za harusi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi