loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

ZSTC yajivunia mafanikio Zanzibar

Alisema shirika litaendelea kugawa faida inayopatikana kutokana na zao hilo kwa kusaidia maendeleo ya jamii kwa kila hali inaporuhusu na fursa inapopatikana ili kujenga imani ya wananchi kuipenda ZSTC na kulipenda zao la karafuu ambapo ndio zao kuu la uchumi Zanzibar.

Bai aliyasema hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika hilo huko Chake Chake katika hafla maalumu ya kuzungumza na wajasiriamali wa Soko la Jumapili ambayo yametolewa na shirika hilo la biashara.

Bai alisema Shirika la ZSTC sasa limeelekeza nguvu zake katika kuisaidia jamii katika shughuli za maendeleo vikiwemo vikundi vya ushirika vya wajasiriamali na wakulima wa zao la karafuu kwa lengo la kuinua uchumi wao.

Alisema miongoni mwa misaada inayotolewa na shirika hilo inaelekezwa zaidi katika miradi ya ujenzi wa barabara za vijijini ikiwemo ya Ng’ombeni Chake na Kiwani, miradi ya ujenzi wa shule, biashara, umeme kwa vituo vya ununuzi wa karafuu na vikundi vya ujasiriamali.

Mapema akizungumza na wajasiriamali wa Soko la Jumapili katika eneo la Chakechake, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla aliwasisitiza wajasiriamali hao kutumia mashamiana hayo na kulitumia soko hilo kuendelea kibiashara.

Alisema Shirika la biashara la ZSTC limefanya jambo la msingi kuwasaidia wajasiriamali hao kutokana na mahitaji yaliyojitokeza ambapo wafanyabiashara hao wamekusanya nguvu zao kukuza uchumi wao.

Amewahakikishia wajasiriamali hao kuwa Serikali ya Mkoa wa Kusini Pemba iko pamoja nao katika kuhakikisha kuwa shughuli wanazoziendeleza sokoni hapo zinaendelezwa kwa maslahi yao na taifa.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mazrouk Khamis-Maelezo Pemba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi