Haki inapogeuzwa silaha, Tanzania na siasa za ICC
DAR ES SALAAM: Kwa miongo kadhaa, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imejiweka kama mwamuzi mkuu wa haki duniani. Lakini katika sehemu kubwa ya Afrika inaonekana sio huru, bali chombo kinachotumiwa dhidi ya viongozi wanaotetea maslahi ya nchi zao yanapogongana na ajenda za mataifa ya Magharibi.
Wakati serikali za wafadhili zinaonyesha kwa njia za chini chini kutoridhishwa na Tanzania, wachambuzi wanatahadharisha kuwa nchi hiyo inaweza kuwa mshambuliaji anayefuata katika mfululizo wa uwajibishaji wa upendeleo ambao tayari umezikumba nchi kadhaa za Afrika.
Mashaka ya waafrika dhidi ya ICC hayakuibuka ghafla.
Kufikia mwaka 2017, baadhi ya viongozi Afrika hawakuridhishwa na ICC , na Baraza la Umoja wa Afrika la Wakuu wa Nchi lilipitisha kile kilichoitwa Mkakati wa Kujiondoa ICC jijini Addis Ababa, likidai kwamba Mahakama ilikuwa imeonyesha mkazo usio sawa kwa mataifa ya Afrika huku ikipuuzia mataifa yenye nguvu na washirika wa karibu wa Magharibi.
Ripoti ya AU ya mwaka huo ilisema ICC imepoteza thamani ya kuanzishwa kwake na sasa inafanya kazi kwa namna inayodhoofisha mamlaka ya Afrika.
Ukosoaji haukupungua kadri miaka ilivyoenda.
Wakati operesheni za kijeshi za Israel huko Gaza zilipozidi kushika kasi, zikipoteza maisha ya raia na kushutumiwa kimataifa, viongozi wa Afrika walihoji kwa nini kasi ile ile ya kumshtaki Rais wa Kiafrika haikuonekana katika mgogoro huo.
Mwanadiplomasia mmoja wa Afrika Magharibi aliiambia jukwaa la kikanda mwaka 2024: “Palestina wanapokufa, kimya kinatawala. Afrika inapodai mamlaka yake, Mahakama inaanza kufanya kazi.”
Tatizo kuu linabaki kuwa utekelezaji wa haki kwa upendeleo.
Marekani, China, Urusi na Israel si wanachama wa ICC lakini zina ushawishi mkubwa duniani. Wakati huohuo, marais, mawaziri na makamanda wa kijeshi kutoka Afrika ndio wanaounda idadi kubwa ya watu waliowahi kushtakiwa na Mahakama hiyo.
Mwanasiasa na msomi wa Kenya, Dk Patrick Lumumba, aliwahi kulitaja jambo hili kwa ukali: “ICC inageuka kuwa fimbo ambayo mataifa makubwa hutumia kuwaadhibu viongozi wa Afrika wasiowatii,”.
Katika mazingira haya, Tanzania inaingia katika kipindi cha mivutano. Udhibiti wake mkali wa rasilimali za taifa, usimamizi wa karibu wa NGOs zinazofadhiliwa na nje, na msimamo wa kuamua njia yake ya maendeleo, kumesababisha baadhi ya serikali za Magharibi kutokuwa na utulivu.
Katika mwaka uliopita, mvutano huu umeonekana kwa namna fiche kusitishwa ghafla kwa misaada, mabadiliko makali ya matamshi ya wafadhili, na taarifa nzito kupitia balozi pamoja na mitandao ya utetezi.
Baadhi ya wachambuzi wa Tanzania wanaona hatua hizi ni mfano wa mifumo iliyojirudia katika nchi nyingine za Afrika: shinikizo huanza si kwa mashtaka rasmi, bali kwa adhabu za kifedha, simulizi za “wasiwasi wa utawala bora.
Mchambuzi mmoja mwandamizi wa usalama wa kikanda alisema kwa ufupi: “Kwanza wanagandisha fedha. Kisha wanapanga kelele. Halafu wanataka uchunguzi. Kinacholengwa si tatizo ni ushawishi.”
Dai kwamba wanaharakati wanaofadhiliwa na Magharibi wanaweza kuyumbisha mazingira ya kisiasa si jipya. Katika Kenya, Ethiopia na Sudan, serikali zimewahi kuishutumu mashirika yanayofadhiliwa na nje kwa kuchochea maandamano, kuathiri maoni ya umma, au kuunda taswira mbaya kimataifa ili kuhalalisha kuingiliwa kwao. Iwe madai haya yanakubalika au hayakubaliki, yanaakisi hofu kubwa zaidi: kwamba nguvu za nje zinashika hatamu za simulizi za ndani.
Kwa upande wa Tanzania, madai kwamba baadhi ya makundi yalipokea ufadhili wa nje katika kipindi kilichoelekea vurugu za karibuni yamezidisha mjadala. Ingawa balozi za Magharibi zinakanusha kushiriki, maofisa jijini Dar es Salaam wanasema mtindo huu unafanana na matukio ya awali ambapo nchi za Afrika zilielekea kwenye mgogoro halafu zikalaumiwa baadaye.
Hofu inayotamkwa kwa faragha na wachambuzi wa usalama na baadhi ya maofisa ni kwamba Tanzania inaweza kuelekezwa kwenye njia inayoishia katika hatua za kisheria za kimataifa. Tayari, sauti kadhaa kutoka Ulaya zimeanza kutaja “uwezekano wa ukiukaji haki” na “haja ya uwajibikaji.” Mlolongo huu, wakosoaji wanatahadharisha, huwa haushangazi.
Nkosazana Dlamini-Zuma, aliyekuwa Kamishna wa AU, ambaye aliongoza msimamo wa bara mwaka 2017, alitoa angalizo kwamba “hakuna kiongozi wa Afrika aliye salama wakati haki inapotumika kwa upendeleo kisiasa.” Onyo hili linarejea leo huku wachambuzi wakihofia kuwa Tanzania inaweza kukumbana na shinikizo la kisiasa linalofichwa kama uangalizi wa kisheria.
Hivyo basi, swali linaibuka: Je, Tanzania inapaswa kuzingatia kujiondoa ICC?
Nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Burundi na Afrika Kusini (ingawa uamuzi wa Pretoria uligeuzwa na mahakama ya ndani) tayari zilishaanza mchakato wa kujiondoa. Rwanda, Ethiopia, Eritrea na nyingine hazijawahi kujiunga, zikisema nguvu ya Mahakama inaweza kutumiwa vibaya.
Mkakati wa kujiondoa wa AU wa mwaka 2017 bado upo, na unaweza kutumiwa na Tanzania kama mwongozo wa kisheria, kidiplomasia na kiutaratibu.
Wanaounga mkono kujiondoa wanasema mamlaka ya taifa lazima yalindwe. Wanakumbusha kauli ya Jopo la Majaji Mashuhuri wa AU kwamba “haki ya kimataifa haiwezi kuwa na uaminifu iwapo inaakisi mizani ya nguvu za dunia.” Kwao, ilhali ICC inashindwa kuchukua hatua dhidi ya mataifa makubwa, haiwezi kudai kutokuwa na upendeleo.
Wanaopinga wanasema kujiondoa kunaweza kuathiri ulinzi wa raia au kudhoofisha mifumo ya uwajibikaji. Hata hivyo, hata wakosoaji wake wanakiri kwamba Mahakama lazima ibadilike ili kurejesha imani ya Afrika.
Kwa wanazuoni wengi wa Kiafrika, hoja kuu si haki yenyewe, bali nani anayeitumia, lini, na kwa maslahi ya nani. Mgogoro wa uhalali wa ICC huzidi kila inapodai kuchunguza nchi zinazoenda kinyume na maslahi ya Magharibi, wakati ikiweka kimya kuhusu washirika wao. Kama mwandishi mmoja wa Afrika Mashariki alivyoandika: “Ikiwa Palestina haiwezi kupata haki The Hague, ni kwa nini mwafrika aamini ataipata?”
Tanzania sasa ipo njia panda. Inaweza kubaki ndani ya ICC na kuhatarisha kuingizwa kwenye malumbano ya kisheria yenye sura ya kisiasa, au inaweza kurejea pendekezo la AU la 2017 na kuangalia mbadala wa kikanda kupitia taasisi za Afrika.
Vyovyote iwavyo, enzi ya mamlaka yasiyoulizwa ya mahakama za kimataifa inaelekea ukingoni. Kinachofuata kitaamua kama haki itakuwa kanuni ya wote au itaendelea kuwa silaha mikononi mwa wenye nguvu.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
NAFURAHI SANA KWA SABABU AMBAO WANAJUA NINI KINAENDELEA (EU) NA ICC INCHI ZA MAGHARIBI ZINATUMIA TAASISI HIZO KAMA KIBOKO CHA KUCHAPIA WAAFRIKA (EU) KIBOKO HICHO HICHO KIMETUMIKA KUICHAPIA TANZANIA WANATAKA KUTUVURUGA KAMA DRC ILI WAWEZE KUPORA MALI ASILI YETU KAMA VILE GESI HELIUM AMBAYO TAYARI WANASAYANSI WAMESEMA KUWA IMEKWISHA GESI IPO USA FUTI ZA UJAZO MILIONI 24 LAKINI GESI HIYO IMEGUNDULIWA TANZANIA MARA MBILI NA ZAIDI (FUTI ZA UJAZO 54 MILIONI) HIVYO NJAMA HIZO NI ZA KUPORA GASI HIYO WATANZANIA TUFUNGUE MACHO YETU TULIONE HILO.