Hakimu Mtwara kortini kwa rushwa ya Sh 50,000

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mtwara, imemfikisha mahakamani Hakimu Mkazi wa Mtwara, Mussa Esanju kwa tuhuma za kupokea rushwa ya kiasi cha Sh. 50,000 kutoka kwa mtuhumiwa aliyefikishwa mbele yake.

Hakimu huyo amefikishwa mahakamani hapo na kusomewa makosa mawili ambayo ni kushawishi kuomba fedha kiasi cha Sh 200,000 na kupokea kiasi cha Sh 50,000, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya  ya Mtwara, Lucas Jang’andu.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mtwara, Enock Ngailo amesema mtuhumiwa alikamatwa Aprili 5, mwaka huu eneo la Mangamba Tanki la Maji majira ya saa mbili usiku, akiwa na fedha ambazo ziliandaliwa maalum na mamlaka hiyo, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mlalamikaji.

Hata hivyo, mshitakiwa baada ya kusomewa mashtaka alikana na kuachiwa kwa dhamana na kesi hiyo itatajwa tena hapo Mei 18, mwaka huu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x