“Hakuna miili zaidi iliyopatikana Hanang”

HANANG, Manyara: SERIKALI hakuna miili zaidi iliyopatikana na hivyo idadi ya miili inabakia kuwa 89 (Watu wazima 50: wanaume 21 na wanawake 29; na watoto 39: kiume 19 na kike 20).

Miili 88 ilishatambuliwa na kuchukuliwa na familia zao kwa ajili ya mazishi lakini mwili mmoja wa mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja bado haujatambuliwa ingawa mchakato wa kuutambua kwa kutumia teknolojia ya vinasaba (DNA) unaendelea.

 

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi , kuhusu maendeleo ya hali baada ya maafa ya maporomoko ya tope, mawe, magogo na maji kutoka Mlima Hanang wilayani Hanang mkoani Manyara, yaliyotokea alfajiri ya tarehe Desemba 03, 2023 imeeleza kuwa mwili wa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu umeshatambuliwa tangu jana kwa kutumia vinasaba na kuchukuliwa na familia yake kwa ajili ya taratibu za mazishi.

 

“Idadi ya majeruhi sasa imebakia sita (6) ambapo watano (5) wapo katika ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara na mmoja (1) katika Hospitali ya Wilaya ya Hanang (Tumaini),” imeeleza taarifa hiyo.

 

Jumla ya waathirika 27 tu kutoka kaya 10 ndio wamebakia kambini na wote sasa wamewekwa kwenye kambi moja ya Shule ya Sekondari Katesh. Kwa ujumla kambi tatu zilizofunguliwa zilipokea na kuhudumia waathirika 534.

 

Hadi sasa 2 Serikali imeshafanikiwa kuwaunganisha na ndugu zao waathirika 472 kutoka kaya 140 na 35 wengine waliondoka wenyewe baada ya kupata mahitaji muhimu; hivyo kufanya jumla ya waliorejea kwa ndugu zao kuwa 507.

 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kusimamia afya kwa umma. Katika juhudi hizi wataalamu wa afya wameshazitembelea kaya 7,393 na kuzipatia vidonge 350,362 vya kutibia maji. Hakuna tatizo la magonjwa ya mlipuko kama kuhara au kipindupindu ambayo hushambulia maeneo ya maafa.

 

Aidha, kwa kutumia wataalamu wa Wizara ya Afya ambao ni wauguzi wawili na madaktari bingwa watatu wa afya ya akili wakiwa na maafisa ustawi wa jamii 91 kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, jumla ya waathirika 3,227 wameshapata huduma ya afya ya akili na kisaikolojia.

 

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button