‘Hakuna mpango kufufua benki ya wakulima Kagera’

NAIBU Waziri wa Fedha, Hamad Chande amesema kuwa Serikali haina mpango wa kuifufua Benki ya Wakulima Mkoa wa  Kagera na badala yake inafanya hatua za ufuatiliaji kuhakikisha suala la ufilisi katika benki hiyo linakamilika.

Chande amesema hayo leo Jumanne Juni 20, 2023 alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Muleba Kusini, Oscar Kikoyo lililohoji Serikali ina mkakati gani wa kuinusuru benki hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya uangalizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

“Kwa mujibu wa sheria ya benki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 benki ikishafutiwa leseni na kuwekwa katika ufilisi hakuna tena uwezekano wa benki hiyo kuwepo na hivyo Serikali haina mpango wa kuifufua benki hiyo,” amesema Chande.

Amesema hadi mwezi Machi mwaka uliopita bodi ya bima ya amana ya benki hiyo imeshalipa fidia ya bima ya amana zinazofikia shilingi milioni 846.11 kwa wateja 1389 waliokuwa na amana katika benki hiyo.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x