“Hakuna mtoto aliyekufa kwa uzembe wa madaktari”

HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke imekanusha taarifa za kifo cha mwanamke aliyefanyiwa upasuaji na kupoteza mtoto kwa uzembe wa madaktari hospitalini hapo.

Katika taarifa yao kwa umma iliyotolewa leo Desemba 18, 2023 hospitali hiyo imeeleza katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita hakuna mtoto aliyezaliwa akiwa na kilogramu 5 hospitalini hapo.

“Hata hivyo picha inayoonekana sio picha ya wodi ya Hospitali ya Temeke na hakuna akina mama wanaolala wawili wawili, kwenye wodi ya matazamio kabla ya kujifungua”

“Wodi hiyo ina jumla ya vitanda 21 na kwa siku akina mama 10-20 hujifungua hapa temeke, hivyo nadra sana kuwa na mlundikano unaolazimu kitanda kimoja kulaliwa na akina mama zaidi ya mmoja.” imeeleza taarifa hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button