Hakuna ofa rasmi mchezaji yoyote Yanga – Walter Harson
DAR ES SALAAM: MPAKA sasa hakuna ofa rasmi kutoka klabu yoyote Afrika inayohusisha usajili wa mchezaji yoyote wa klabu ya Yanga, Meneja wa Yanga, Walter Harson ameeleza.
Hivi karibuni ziliibuka tetesi kiungo wa timu hiyo Stephen Aziz Ki kuhusishwa na klabu ya Far Rabat ya Morocco, na kipa Djigui Diarra kuhusishwa kuondoka.
Akizungumza na mwandishi wetu, Walter Harson amesema ni kawaida hasa ligi zinapoelekea ukingoni wachezaji wakubwa kuhusishwa kuondoka ila mpaka sasa hakuna klabu ambayo imeweka ofa mezani kuhitaji huduma ya mmoja wa wachezaji wao.
“Yote haya yanatokana na utendaji mzuri ambao tumekuwa nao kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu, baadhi ya wachezaji kuwa na viwango vizuri,” amesema Walter.
Amesema timu yoyote itahitaji huduma ya mchezaji yoyote uongozi wa klabu utakaa na kuona nini kinaweza kikafaa kwa wakati huo, kama kuwapa fursa kujaribu sehemu nyingine watawapa kama kusalia watasalia hivyo naamini viongozi wao ndio wanamajukumu makubwa,” amesema Walter.