Hakuna visa kuingia Kenya

KENYA; Nairobi. Kenya inatarajiwa kuwa nchi isiyo na visa mwanzoni mwa mwaka 2024.
Rais wa Kenya, Wiliam Ruto amesema hakuna ulazima mtu yoyote kuwa na mzigo wa kupambania mchakato wa kupata visa ili kuingia nchini humo.
Akizungumza leo Desemba 12, 2023 maadhimidho ya siku ya Uhuru wa Kenya, Ruto amesema hatua hiyo inalingana na ahadi ya Kenya ya kukomesha hitaji la wasafiri wanaoomba visa kuzuru Kenya.
Ili kutekeleza sera hiyo mpya, Ruto amesema wameunda mfumo mpya wa kidijitali ambao utahakikisha wasafiri wote wanaokwenda Kenya wanatambuliwa mapema kwenye jukwaa la kielektroniki.
“Wasafiri wote watapata idhini ya kusafiri kielektroniki ni furaha kubwa kama Rais wa nchi hii isiyo ya kawaida kutoa tangazo la kihistoria la uamuzi wa Serikali ya Kenya,” amesema Ruto.

Habari Zifananazo

Back to top button