‘Hakuna wanyama wanaosafrishwa nje’

‘Wenye mapenzi na uandishi wakasome’

WATANZANIA wametakiwa kupuuza taarifa zinazosambazwa mitandaoni kuwa kuna wanyama wanaosafirishwa na ndege zinazotua katika hifadhi za wanyama.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Januari 15 jijini Dodoma akizungumza na waandishi wa habari, ikiwa ni muendelezo wake wa Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali na kusema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imejipambanua katika kukuza sekta hiyo.

“Hivi karibuni kulikuwa na uzushi kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna ndege zinakwenda kwenye hifadhi zetu, zinabeba wanyama. Tupuuze hizo taarifa, hakuna ndege inayokwenda kwenye hifadhi zetu na kubeba wanyama.

Advertisement

“Ndege zinazokwenda kwenye hifadhi zetu zinapeleka watalii na mizigo ya watalii. Hakuna mnayama aliyesafirishwa. Nchi yetu bado imesitisha usafirishwaji wa wanyama. Wanyama wetu wako salama sana,” amefafanua Msigwa.

Amesema kuwa sekta ya Utalii kwa ujumla imekua na inaendelea kuimarika na watalii wanaongezeka baada ya sekta hiyo kuathiriwa na ugonjwa wa Uviko-19 ulioukumba dunia mwaka 2020 na kusababisha sekta hiyo kudorora kwa kipindi kirefu.

“Idadi ya watalii inaongezeka kwa kasi kubwa baada ya juhudi binafsi za Rais Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya The Royal Tour. Idadi ya watalii imepanda mpaka kufikia 1,405,449 kutoka watalii 922,692,” amesema.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *