LINDI: Magari ya mizigo, mabasi na magari mengine madogo, yaliyokwama kwa siku 6 katika barabara ya Lindi – Dar es Salaam, eneo la njia nne (Mikereng’ende) hadi Somanga yakitokea Lindi kuelekea Dar es Salaam, yameanza kuruhusiwa kupita kuendelea na safari.
Magari hayo yameanza kupita baada ya kukamilisha kwa urejeshwaji wa mawasiliano katika maeneo ya Mikereng’ende, Songas na Somanga ambayo yalikatika kutokana na mvua zilizonyesha, na kuambatana na Kimbunga Hidaya.
Akisimamia zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack, amewataka wasafiri, wasafirishaji na watumiaji wengine wa barabara, kusafiri kwa tahadhari ambapo maeneo mengine yanaendelea na matengenezo.
http://Isome pia:https://habarileo.co.tz/mawasiliano-barabara-lindi-dar-yarejea/
Aidha, Kazi ya urejeshaji wa miundombinu ya barabara ya Lindi – Dar es Salaam eneo la Nangurukuru, ipo katika hatua ya ukamilishaji.
Kupitia ukurasa wa Instagram Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa ameandika ” Tunarudi kwenye hali ya ushwari. Matengenezo yanaendelea huku wasafiri na wasafirishaji wakiendelea na safari. Asante sana Mwenyezi Mungu.