Hali ya Pele yaanza Kuimarika, adai yuko Imara

NGULI wa soka wa Brazil, Edson Arantes do Nascimento ‘PELE’ amesema kwa sasa “najisikia imara” ni baada ya siku kadhaa zilizopita kulazwa hospitalini na jana kuingizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na shida ya upumuaji.

“Niko imara na matumaini mengi, naendelea kufuata utaratiu wa matibabu kama kawaida” aliandika Pele kwenye ukurasa wake wa Instagram. Gwiji huyo wa soka mwenye umri wa miaka 82 aliwataka mashabiki kuwa watulivu na kuwaza chanya.

“Nina imani nyingi katika Mungu na kila ujumbe wa upendo ninaopokea kutoka kwenu kote ulimwenguni hunifanya niwe na nguvu nyingi,” aliongeza Pele.

Ijumaa madaktariwalisema mkongwe huyo alipata nafuu na kuwa katika hali nzuri kufuatia kufanyiwa uchunguzi. Pele, ambaye alikuwa na uvimbe na matatizo ya moyo baada ya kulazwa hospitalini wiki hii, aligunduliwa haswa na matatizo ya upumuaji, ESPN Brasil iliripoti hapo awali.

Binti wa Pele, Kely Nascimento, alisema baba yake awali alikuwa amelazwa hospitalini ili kudhibiti dawa zake zinazohusiana na matibabu yake ya saratani.

Habari Zifananazo

Back to top button