Halmashauri yazika marehemu 52 Morogoro

SERIKALI wilayani Morogoro kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro umelazimika kuwazika marehemu 52 wasio na ndugu kwenye makaburi ya Kola katika kipindi cha mwaka 2022/23.

Meya wa Manispaa hiyo, Pascal Kihanga alisema hayo mjini Morogoro katika mkutano wa kawaida wa mwaka wa Baraza la Madiwani wa halmashauri manispaa hiyo.

Kihanga alisema watu wasiokuwa na ndugu wanapokufa na kukaa hospitalini zaidi ya siku 20 halmashauri za jiji au manispaa huwazika.

Advertisement

Kihanga alisema kuwa kati miili hiyo wapo wanaume 40, wanawake 11 na fuvu la kichwa lililookotwa Machi 21 mwaka huu katika Kata ya Bigwa na lilizikwa Aprili mwaka huu.

Katika hatua nyingine watu 187 waling’atwa na mbwa kipindi cha mwaka 2022/23 na kati ya hao 103 walipatiwa chanjo ya kichaa cha mbwa baada ya kujiridhisha kuwa na uwezekano mkubwa mbwa waliong’atwa walikuwa na kichaa cha mbwa.

Kihanga alisema wengine 84 walipatiwa chanjo ya pepopunda baada ya kujiridhisha kuwa mbwa hao waliowang’ata hawakuwa na uwezekano wa kuwa na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.

“Hawa watu 84 waliwambiwa kwenda kuwaagalia mbwa waliowang’ata kwa siku 10 kama bado wapo hai…na wagongwa wengi zaidi ya 38 waliong’atwa na mbwa walitoka kata ya Kihonda,“ alisema Kihanga.

Katika hatua nyingine baadhi ya madiwani ameshauri viongozi wa serikali na wanasiasa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuzingatia usafi na utunzaji wa mazingira ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.

Diwani wa Kata ya Mji Mpya, Emmy Kiula alishauri elimu itolewa kwa wanawake watumie taasisi zilizosajiliwa kukopa fedha badala ya vikundi visivyotambulika au kusajiliwa kwa kuwa vinatoa mikopo unayoitwa mikopo umiza (Kausha Damu) na kuwaingiza katika changamoto za urejeshaji.

“Tushirikiane kutoa elimu kwa wanawake ambao ndiyo wakopaji kwenye vikundi ambavyo havijali makubaliano yanayofikiwa… tuwashauri wakope kwenye vikundi vilivyosajiliwa na vyenye kuwa na utaratibu mzuri,“ alisema Kiula

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *