Halmashauri zakumbushwa kutekeleza agizo la Rais Samia

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka halmashauri zote nchini kutekeleza agizo la Raisi Samia la kujenga wodi muhimu mbili katika vituo vyote vya afya nchini.

Kwa mujibu wa Majaliwa, Rais alitoa maelekezo kwenye vituo vya afya baada ya kukamilika lazima kuwe na wodi mbili , wodi moja ya mama na mtoto na wodi nyingine ya wanaume ya magonjwa mchanganyiko.

Majaliwa ametoa maagizo hayo leo mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya Kata ya Kitama Wilaya ya Tandahimba, Mkoani Mtwara.

Amezitaka halmashauri hizo kujenga wodi hizo kutumia mapato ya halmashauri na kuacha tabia ya kukaa kusubiria serikali kuu kutoa pesa.

Majaliwa amefika Mkoani Mtwara jana (Agosti 12) kuendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kutembelea na kukagua miradi, kuona utekelezaji, ubora wa miradi na kama imejengwa Kwa thamani ya pesa.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button