Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro raha tu

ARUSHA: Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro imekamilisha ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya halmashauri hiyo kwa asilimia 88 huku ujenzi wake ukiwa umetengewa kiasi cha Sh bilioni 2.6

Akizungumza kwenye ziara inayofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella wilayani Ngorongoro msimamizi wa mradi huo ,Injinia Masasila Chigulu amesema mradi huo ulianza Machi,2021 na unatarajiwa kukamilika Novemba ,2023.

Injinia Chigula amesema ujenzi huo unahusisha miundombinu ya ofisi za halmashauri,uzio,ujenzi wa Nyumba za walinzi, nyumba ya kusambazia umeme, maegesho ya magari, barabara pamoja na taa za ulinzi

“Mradi umekamilika kwa asilimia 88 lakini tunakabiliwa na mazingira magumu ya usafirishaji wa vifaa vya ujenzi hali inayopelekea kupunguza kasi ya utekelezaji wa mradi huu”amesema

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amepongeza Mkurugenzi wa halmshauri hiyo,Nassoro Shemzigwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Raymond Mangwalla kwa kusimamia vema ujenzi wa jengo hilo ambali awali lilikuwa likisuasua kuendelea kwake.

Rc, Mongella amesisitiza nidhamu,usimamizi mzuri wa miradi sanjari na ufuatiliaji wa karibu wa mambo mbalimbali ya kimaendeleo ndio unaopelekea miradi ya kimaendeleo kukamilika kwa wakati ikiwemo ushirikishwaji wa wataalamu ili kusogeza huduma za maendeleo kwa wananchi.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button