Hamilton kujiunga Ferrari

MKALI wa mbio za magari wa Uingereza, Lewis Hamilton ataondoka timu ya Mercedes na kujiunga na Ferrari kwa msimu wa 2025, Sky Sports News inaeleza.

Inafahamika kuwa Mercedes imetaarifiwa na mtendaji mkuu wa timu hiyo, Toto Wolff, kabla ya tangazo rasmi baadaye leo.

Hamilton, ambaye ameshinda rekodi ya pamoja ya ubingwa wa dunia mara saba, amekuwa na Mercedes tangu mwaka 2013.

Advertisement

Kabla ya hapo, Hamilton mwenye umri wa miaka 39 alikuwa McLaren.