‘Nachukia wanaoniomba niwazalie’
MSANII Hamisa Mobetto, ambaye pia ni mama wa watoto wawili amesema anachukizwa na baadhi ya wanaume wanaomfata na kumuomba awazalie watoto.
Hamisa amesema baadhi ya wanaume wamekuwa wakimfuata na kumueleza kuwa wanataka awazalie watoto na kudai kuwa kama mtu anataka amchukie maisha amfuate amwambie kauli hiyo.
“Ukitaka nikuchukie maisha njoo niambie kauli hiyo ya nizalie mtoto nitakuchukia sana na kukublock kila sehemu,”amesema Hamisa na kuongeza:
“Mimi ni mama wa watoto wawili, nilizaa na watu ambao hawakuniambia kauli hizo, ilitokea. Nifuate kwa kunioa watoto majaliwa ya Mungu.”