Harakisheni ukarabati Sheikh Amri Abeid – Ndejembi

ARUSHA: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Deogratius Ndejembi ameagiza kufikia Aprili 15 mwaka huu, ukarabati wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uwe umekamilika ili kutumika katika sherehe za Mei Mosi.

Ndejembi ameyasema hayo wakati wa kikao cha pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) alipokagua maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kikao hiko kimehudhuriwa  na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, Katibu Mkuu wa Wizara, Mary Maganga pamoja na viongozi wa shirikisho hilo wakiongozwa na Rais wao, Tumaini Nyamhokya.

Habari Zifananazo

Back to top button