NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘ Harmonize’ amesema ana mpango wa kutengeneza filamu kuelezea maisha yake ya muziki.
Akizungumza na HabariLEO, msanii huyo ameeleza muziki unahistoria katika maisha yake ndio maana anataka kutengeneza kumbukumbu ya kudumu.
“Kuna mengi niliyopitia na wapo wengi wamechangia mimi kufika hapa nilipo ndio maana nataka kutengeneza filamu itakayozungumzia maisha yangu ya muziki,” alisema Hamornize.
Msanii huyo ameeleza kuwa pamoja na changamoto zote alizopitia lakini anajivunia kuwa mpambanaji katika kipindi chote tangu anatoka kupitia muziki.
Alisema anamshukuru Mungu kwa mafanikio aliyokuwa nayo lakini hayamfanyi aridhike sababu bado ana malengo ya kufika mbali zaidi ya alipo sasa
Hamornize ni miongoni mwa wasanii walioibukia kwenye Lebo ya ‘WCB’ inayomilikiwa na msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ kabla ya kujitoa na kuanzisha Lebo yake ya Konde Gang ambayo inafanya vizuri pia.