Hatma ya Mnyama leo
HATMA ya Simba SC itajulikana leo ambapo timu hiyo itacheza na Al-Ahly mchezo wa marudiano wa African Football League nchini Misri majira ya saa 11:00 jioni.
–
Mnyama anaingia kwenye mchezo huo akiwa na kumbukumbu ya mchezo wa kwanza uliosha sare ya mabao 2-2 uwanja wa Mkapa.
–
Shirikisho la soka Afrika (CAF) wameeleza kanuni za mashindano hayo hakuna goli la ugenini, hivyo timu itakayofunga idadi itakayomzidi mpinzani itasonga hatua nyingine.
–
CAF wamesema kwa hatua ya robo na nusu, mchezo ukiisha sare baada ya michezo yote miwili, hakutakuwa na dakika za nyongeza ‘extra time’ mchezo utaenda kwenye penalty.
–
Mchezo mmoja tu wa fainali ndiyo utakuwa na muda wa nyongeza wa dakika 15 endapo mchezo huo utaenda sare baada ya dakika 90. Matokeo yakibaki sare mchezo utaenda penalty.