WAJUMBE wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha kutoka wilaya saba leo wanapiga kura kumchagua mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha baada ya aliyekuwa mwenyekiti, Zelothe Stephen kufariki Dunia.
Uchaguzi wa kujaza nafasi ya mwenyekiti ajaye unafanyika leo jijini Arusha ambapo wajumbe wataamua nani awe mwenyekiti wa chama hicho.
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi huo, Anthony Mtaka ambapo wajumbe mbalimbali wataamua hatma ya mwenyekiti wa chama hicho mkoani huo ambapo ameambatana na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Halima Mamuya
Wagombea wanaowania uenyekiti huo ni Dk,Daniel Pallangyo,Loy Sabaya,Solomon Kivuyo na mwanamke pekee ambaye ni Edna Kivuyo.
Comments are closed.