‘Hatua zinachukuliwa kulinda thamani ya shilingi’

SERIKALI imesema inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kulinda thamani ya shilingi ya Tanzania.

Akijibu swali la Mbunghe wa Mbogwe, Nicodemus Maganga aliyetaka kujua mpango wa serikali katika kuongeza thamani ya Shilingi ya Tanzania, Waziri Wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, ametaja baadhi ya hatua hizo ni kushirikisha sekta binafsi katika kuimarisha mikakati ya kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi.

“Kuhimiza wananchi kuongeza matumizi ya bidhaa na huduma zinazozalishwa hapa nchini ili kupunguza mahitaji ya fedha za kigeni, kusimamia kwa karibu wazalishaji wa ndani ili kuongeza ubora katika uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa lengo la kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

“Kuendelea kusimamia utekelezaji wa kifungu 7(3) na 13(1) cha Kanuni za Fedha za Kigeni za mwaka 2022, zinazoelekeza wafanyabiashara kuweka katika benki zilizopo nchini fedha za mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi ndani ya siku 90 tangu siku ya kusafirisha bidhaa au kutoa huduma na wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kutoka nje kufanya malipo kwa kutumia benki na taasisi nyingine za fedha zilizopo nchini.

“Kuongeza vyanzo vya upatikanaji wa fedha za kigeni ikiwemo ununuzi wa dhahabu; vi. Kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji kutoka nje.

“Kusimamia utekelezaji wa sera ya fedha ili kuhakikisha utulivu wa mfumuko wa bei nchini,” amesema Waziri Nchemba.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button