KUNA dalili kuwa huenda Kai Havertz akasepa Chelsea, baada ya Arsenal kuwasilisha ombi lingine la kumsajili Mjerumani huyo.
Imeelezwa Arsenal imerudi tena kwa Havertz wakiwa na dau la £65m.
Mazungumzo yatafuata baina ya timu hizo kuhusu dau hilo jipya.
Havertz amekuwa muazi kwamba anataka kuondoka Stanford Bridge kwenda Arsenal, kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo, Fabrizio Romano.
Awali Chelsea walitaka £75m Arsenal iligoma kutoa pesa hiyo.